Paris- Chama cha kisosholisti cha Ufaransa kimepata viti vingi katika bunge la chini kwenye uchaguzi wa duru ya pili siku ya jumapili.Imefahamika kuwa chama hicho kimepata viti 291 kati ya 577 na hivyo kukifanya kuwa na uwezo wa kupitisha miswada ya kuongeza ushuru na kufanyia mabadiliko makubaliano ya ulaya ya kubana matumizi.Matokeo hayo pia yatampa nguvu rais wa Ufaransa Francois Hollande kufanyia mabadiliko sheria za kufanya kazi, mfumo wa elimu na mabadiliko ya fedha ili kusaidia ukuaji wa uchumi nchini humo.