Chelsea hatimaye imemteua Roberto Di Matteo kama meneja wake wa kudumu kwa kutiliana saini mkataba wa miaka miwili.

ashinda FA na Ulaya
Meneja huyo aliyekua kiongozi wa MK Dons na pia West Brom, Di Matteo alipoteza mechi tatu tu kati ya mechi 21 alizosimamia, na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu waliunga mkono ateuliwe kama meneja wa kudumu hususan baada ya kushinda kombe lililoikwepa klabu hio kwa mda mrefu la Mabingwa wa Ulaya.