KANUMBA ALIJITABIRIA KIFO CHAKE
By Maganga Media - Apr 15, 2012
Filamu hiyo aliyoitengeneza marehemu Kanumba mwenyewe ambayo bado haijaingia sokoni, mwanzoni ilikuwa inaitwa Love of Price lakini baadaye Kanumba aliibadilisha jina na kuiita Love & Power.
Kwa mujibu wa mwandishi wa muswada (script) wa filamu hiyo, Ally Yakuti, mazingira ya kifo cha Kanumba kwenye muvi hiyo yanafanana na kilichomtokea usiku wa kuamkia April 7, mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar.
STORI ILIVYO
Stori ya filamu hiyo inaonyesha kuwa Edwin (Kanumba) alitokea kumpenda mwanamke lakini kwa kuwa yeye alikuwa maskini, ‘demu’ huyo aliyetumia jina la Christina (Irene Paul) kwenye filamu hiyo alimkataa akidai kuwa hana hadhi.
Alisema kuwa wakati Edwin (Kanumba) anaendelea kumfuatilia, akasikia kuwa mwanamke huyo anaumwa na kupona kwake lazima ipatikane figo ya mtu mwingine ili awekewe.
Stori inaendelea kutiririka kuwa Edwin (Kanumba) anajitolea kutoa figo yake moja. Muvi hiyo inaonesha kuwa baada ya kupona, Christina (Irene Paul) anagundua kuwa mwanaume ambaye hamtaki kwa sababu ya umaskini wake, ndiyo aliyenusuru maisha yake kwa kumtolea figo. Stori inaendelea kuonesha kuwa katika hali hiyo, mwanamke huyo anakuwa hana jinsi hivyo anakubali kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Edwin (Kanumba).
ASUKUMWA, AFA PAPO HAPO
Katika filamu hiyo kuna kipande kinaonesha kuwa baada ya wawili hao kuishi kwa muda mrefu katika hali ya umaskini, Christina (Irene Paul) anashindwa maisha hayo, anambwaga Edwin (Kanumba) na kuwa na mwanaume mwingine.
Muvi hiyo inaendelea kuonesha kwamba kwa kuwa Kanumba alimpenda mwanamke huyo, hakukubali aondoke na katika kumzuia, ndipo mwanamke huyo alipomsukuma na kujigonga ukutani kisha akadondoka na kufa papohapo.
DAKTARI HUYO HUYO
Katika hali ya kushangaza, stori ya muvi hiyo inaonesha kuwa daktari ambaye anaonekana akimpima Edwin (Kanumba) kwenye filamu hiyo anayejulikana kwa jina maarufu la Kidume ndiye huyohuyo aliyempima Kanumba alipodondoka na kufariki dunia kiukweli usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
ALIYEMPELEKA MOCHWARI
Msanii wa filamu za Kibongo, Idrisa Makupa ‘Kupa’ ambaye kwenye filamu hiyo anaonekana akishiriki kumpeleka Edwin (Kanumba) mochwari, ndiye huyohuyo aliyeshiriki zoezi kama hilo la kumpeleka Muhimbili huku akimfumba macho baada ya kufariki kiukweli.
IRENE PAUL ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa juu ya ishu hiyo, mwigizaji Irene Paul ambaye kwenye filamu hiyo alitumia jina la Christina akionekana akimsukuma Edwin (Kanumba) na kufariki, alisema kifo cha staa huyo kimekatisha ndoto zake kwani ndiye aliyemwingiza kwenye filamu hivyo aliposikia habari hiyo mbaya ya kufa, mbali na kuzimia amekuwa akihisi bado ni ndoto.
“Kweli kwenye ile filamu nilimfanyia Kanumba mambo yote ambayo yamekuja kuwa ya kweli,” alisema Irene Paul akiangua kilio.
MASWALI TETE
Baada ya kujiridhisha na matukio yote ya kwenye filamu na uhalisia wa kifo cha Kanumba ndipo yaliboibuka maswali tete kuwa, je, Kanumba alifahamu juu ya kifo chake kwani kila kitu kipo kwenye filamu hiyo? Au ni nini kilichokuwa kikimtuma kufanya matukio yaliyoashiria tukio hilo?
TUJIKUMBUSHE
Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi ya Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake na kuzikwa Aprili 10 katika makaburi ya Kinondoni, Dar.
Swali moja la kujiuliza juu ya hilo ni je, wasanii waache kutunga nyimbo na maigizo juu ya maisha yao au nini kifanyike? Toa maoni yako hapa chini.
MAONI YA WASOMAJI KUTOKA FACEBOOK
- Mwanya Major Josue Ninaweza kusema alijitabilia kifo kwasababu alikua anatunga ki2 ambacho kinataka kutokea na kikatokea ndo rai yangu ok.
- Joyce Sendwa Hatuwez cema wasanii wastop.coz they are acting..ila cna iman kama kila ulifanyalo una hakika laja kama lilivyo...ni vigum mtu kuwa na hakika kwamb kesho ntakufa coz of thc.tenx
- Loveness Msangi Tukio hilo lic wakatishe wasanii tamaa ya kuendelea na kaz yao kwan lililopangwa kutoke litatokea 2 hata kama hawata onyesha kwenye film zao.
- Zakayo Mmbaga siwezi nikakubali moja kwa moja kwa sababu ni filamu nyingi ka act za matukio kama hayo b4 lkn haikuwa ivyo. its God wil
- Esther Lyimo Ata kama ingekua cio kujitabria lakn kanumb cku zake za kuish apa dunian zilikua zimeisha.akuna kujitabiria wa kusukumwa.kafa kama wazazi wangu na wa2 wengne.mungu awasehem.
- Sato Abel Ebwana hii blog inatisha,lakini hii isituchukulie muda kwani kunamsemo wa kisukuma(ochaga atagayaga nogi)16 hours ago · ·
2
- Kabebitho Victorious kila kitu ni mpango wa MUNGU kwa aaminiye so ilipangwa kutokea na ni wengi wameimba na kutunga but still wapo though most of time inakuwa kweli but isiwe kigezo cha kuwazuia wasanii kutunga6 minutes ago · ·
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII